{ "guidelines.title": "Miongozo ya Jumuiya ya Scratch", "guidelines.header": "Tunahitaji msaada wa kila mtu ili tukuze Scratch iwe ya kupendeza na jamii ya ubunifu ambapo watu wenye asili na masilahi tofauti wanahisi wamekaribishwa.", "guidelines.respectheader": "Kuwa na heshima.", "guidelines.respectbody": "Wakati wa kushiriki miradi au kutuma maoni, kumbuka kuwa watu wa umri na malezi tofauti tofauti wataona kile ulichoshiriki.", "guidelines.constructiveheader": "Kuwa yenye faida", "guidelines.constructivebody": "Wakati wa kutoa maoni kuhusu miradi ya wengine, zingatia jambo unalopenda kuhusu mradi huo na upeane mapendekezo.", "guidelines.shareheader": "Shiriki.", "guidelines.sharebody": "Uko huru kurekebisha miradi, maoni, picha, au kitu kingine chochote kilicho kwenye Scratch – na mtu yeyote anaweza kutumia chochote kile unachoshiriki. Hakikisha unawatambua na kuwahongera wengine wakati unapobadilisha au kuboresha miradi yao", "guidelines.privacyheader": "Hifadhi taarifa ya kibinafsi faraghani", "guidelines.privacybody": "Kwa sababu za kiusalama, usitoe taarifa yoyote ambayo inaweza kutumika kwa mawasiliano ya kibinafsi - kama vile majina ya mwisho, nambari za simu, anwani, anwani za barua pepe, viungo kwenye wavuti za kijamii au tovuti zilizo na gumzo ziisizothibitishwa.", "guidelines.honestyheader": "Kuwa mwaminifu.", "guidelines.honestybody": "Usijaribu kujifanya kuwa mwanascratch mwengine, wala usieneze uvumi, au kujaribu kutunga hila za kuwahadaa wanajamii.", "guidelines.friendlyheader": "Saidia kukuza urafiki katika tovuti.", "guidelines.friendlybody": "Ikiwa unahisi kuwa mradi au maoni ni dhalimu, inadunisha, inatukana, inasababisha uhasama au vinginevyo visivyofaa, bonyeza “Ripoti” kutujulisha kuhusu hilo.", "guidelines.footer": "Scratch inawakaribisha watu wote wa umri, kabila, dini, ulemavu, tabaka, maelekeo ya kingono na utambulisho wa kijinsia." }